Mgombea Urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema kuwa endapo chama hiko kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi ,kitaanza mchakatao wa kubadili katiba ndani siku 100 baada ya kuapishwa .

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari mkoani Arusha .

“Nikichaguliwa Rais nitaunda Serikali ya Chadema kwasababu ya Katiba inavyosema. kama kutakuwa na uhitaji itabidi tubadilishe katiba kwanza, na moja ya maazimio ya Chadema ikishinda uchaguzi Mkuu ndani ya siku 100 tutaanzisha mchakato wa Katiba mpya.” amesema Lissu

Aidha, Lissu amedai kwamba Watanzania wapo tayari kuipigia kura CHADEMA kwenye nafasi ya urais, ubunge na udiwani na kila mahali ambako amekwenda amepokelewa na amehutubia mikutano ya maelfu ya Watanzania na kati yao hakuna hata mmoja aliyehitaji kuhongwa.

Kwa kauli hii, Manchester United hawana chao
Trump, Biden watupiana vijembe