Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu leo Agosti 8,2020 atafika katika ofisi za NEC jijini Dododma kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa katika nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene, amesema zoezi  la kuchukua fomu litaambatana na shughuli za kutafuta wadhamini ambapo leo wataanzia katika ofisi za kanda ya kati zilipo jijini Dodoma.

Makene amesema kuwa baada ya shughuli zote hizo kumalizika,Kesho Agosti 9, 2020 watahamia katika mkoa wa Singida kwa ajili ya kuendelea na zoezi la kutafuta wadhamini, lakini pia itahusisha ujio wa Lissu katika eneo alilozaliwa tangu alipoondoka baada ya kushambuliwa na risasi.

“Shughuli zitaanza leo hakuna kitu kitalala na baada ya kuchukua fomu tutatafuta wadhamini ambapo leo ni hapa Dodoma baada ya hapo tutahamia Singida, tutatafuta wadhamini na pia ni ‘home coming’ ya Tundu Lissu na itakuwa ni siku mbili mana ni nyumbani baada ya jaribio la mauaji dhidi yake’’amesema Makene.

Zoezi hilo litahusisha viongozi na wanachama  wa CHADEMA ambapo Tundu Lissu ataambatana na Mgombea Mwenza Salum Mwalim pamoja na wananchi wengine watakaojitokeza.

SADC ngazi ya makatibu wakuu wajadili kuboresha rasimu za nyaraka za kisera
NCCR-Mageuzi urais Zanzibar yatoka kapa