Mgombea Urais kupitia chama cha ACT wazalendo Bernard Membe ,ameiomba tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) itumie busara katika uamuzi wa rufaa za vyama vya upinzani zilizopo katika tume hiyo .

Membe amesema hayo alipokuwa akihutubia Mkutano wa kampeni katika eneo la Ikwiriri wilayani Rufiji mkoa wa pwani .

“Naiomba Tume ya Uchaguzi (NEC) itende haki ,itumie busara katika maamuzi yao kuhusu rufaa za vyama vya upinzani zilizopo NEC,” Amesema Membe .

Amesema NEC inapaswa kutenda haki katika kushughulikia suala la rufaa za vyama vya upinzani .

Hoja hiyo imeungwa mkono na mgombea wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Tundu Lissu , kuwa tume isimamie uchaguzi kwa vyama vyote na iwarudishe haraka wagombea wa vyama vya upinzani .

“Naomba niunge mkono wito wa mwenyekiti wa warudishe haraka iwezekanavyo wagombea wetu wote walioenguliwa hovyo ili waweze kuwa wagombea katika uchaguzi huu,”

Lissu amesema hayo akihutubia wafuasi wa CHADEMA mkoani Tabora

Kombe la AFCON lapotea
CHADEMA, TBC mambo safi