Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu amethibitisha kuwa ni kweli ana tiketi ya ndege ya kuondoka nchini Disemba 18, 2020 kwenda Ubelgiji.

Lissu amesema kuwa ataenda kutokana na matatizo ya kiafya aliyoyapata baada ya kupigwa risasi mwaka 2017 akiwa mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa Lissu, Daktari wake amemuambia Disemba 20 arudi Ubelgiji ili akaangalie maendeleo ya afya yake.

Lissu amesema hayo akijibu tetesi kuwa kuna baadhi ya wagombea wana tiketi za ndege ili wakimbie wakisababisha fujo nchini.

JPM azindua treni Arusha
NEC yatoa ufafanuzi Lissu kuzuiwa kufanya kampeni