Mbunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema kuwa hawezi kuacha kuitafuta haki pamoja na kuikosoa serikali pindi itakapoenda kinyume na utaratibu wa kuongoza nchi.

Ameyasema hayo akiwa Hospitali jijini Nairobi nchini Kenya anakopatiwa matibabu tangu mwezi Septemba 2017, alipojeruhiwa mkoani Dodoma kwa kushambuliwa na watu wasiojulikana.

”Siachi kuikosoa Serikali hata siku moja, nitadai haki hadi mwisho wa maisha yangu, nimekuwa na tabia ya kudai haki tangu nikiwa mdogo nafanya hivyo ili kuokoa Taifa langu,” amesema Lissu.

Hata hivyo, ameongeza kuwa yupo katika hali nzuri, amepona majeraha yote kilichobaki kusimama na kutembea, huku akihoji vyombo vya dola kukaa kimya akiwemo Spika wa Bunge, Jaji Mkuu wa Tanzania pamoja na Mahakama.

 

Mugabe na mkewe waondoka Zimbabwe
Bashe: Sisi tulijaribu tukashindwa UVCCM