Meli ya MV Mwanza “Hapa Kazi Tu” iliyojengwa kwa gharama ya zaidi ya bilioni 109 imeshushwa majini katika Ziwa Vitoria Jijini Mwanza kwa ajili ya majaribio na kukamilisha ujenzi wake.
Tukio hilo la kihistoria la kushushwa kwenye maji kwa meli hiyo inayojengwa katika Bandari ya Mwanza Kusini litaongozwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa huku likishuhudiwa na mamia ya wakazi wa Mwanza.
Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 1, 200, tani 400 za mizigo na magari 20 yakiwemo makubwa matatu inajengwa na mkandarasi kutoka Kampuni ya Gas Entec Ship-Building Engineering na Kang Nam Corporation za Nchini Korea kwa kushirikiana na Suma Jkt.
Meli hiyo ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 82 huku ikitarajiwa kukamilika ifikapo Agosti, mwaka huu safari zake itafanya kati ya Bandari za Mwanza, Kemondo, Bukoba, Portbail nchini Uganda na Kisumu nchini Kenya.