Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn amewasili nchini leo Machi 31, 2017 ambapo atakuwa nchini kwa shughuli mbalimbali za kidiplomasia zinazogusa nyanja muhimu za kiuchumi, Biashara, na Ushirikiano baina ya Nchi ya Ethiopia na Tanzania.
Pia atasaini mikataba mitatu, Kutembelea bandari na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli.
Moja kwa moja kutoka Ikulu jijini Dar es salaam Waziri huyo pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kufanya mazungumzo. Bofya hapa kutazama
Ugeni huo utaipa Tanzania fursa ya kujifunza mambo mengi kupitia kwa ugeni huo juu ya kukabili changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya kilimo cha kisasa katika maeneo yenye uoto wa asili wenye changamoto kama milima hapa nchini Tanzania.
Bofya hapa kutazama