Leo Aprili 26, 2017 ni siku ya maadhimisho ya miaka 53 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, sherehe ambazo kitaifa zinafanyika mkoani Dodoma na mgeni rasmi ni Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa mnamo tarehe 26 Aprili, 1964 kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (inayojumuisha Visiwa vya Pemba na Unguja).
Mkataba huu wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume tarehe 22 Aprili 1964 huko Zanzibar. Mkataba huo ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi hapo tarehe 26 Aprili, 1964 na mnamo tarehe 27 Aprili, 1964, viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam na kubadilishana Hati za Muungano.
Tazama hapa moja kwa moja kutoka Dodoma, Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzaibar
Tazama ndege za kijeshi zilivyo pamba maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Dodoma