Majogoo wa jiji Loverpool wanajiandaa kukamilisha mpango wa kumpa ajira meneja kutoka nchini Ujerumani, Jurgen Klopp, baada ya kuhitimisha sehemu ya kwanza ya mazungumzo.

Taarifa za awali zinaeleza kwamba pande hizo mbili zimeshakubaliana baadhi ya mambo muhimu, ambayo yatakuwa kichocheo cha meneja huyo kufanya kazi huko Anfield kama mbadala wa Brendan Rodgers ambaye alionyeshwa mlango wa kutokea mwishoni mwa juma lililopita.

Uongozi wa Liverpool, kesho unatarajia kukutana na waandishi wa habari, kwa lengo la kumtambulisha rasmi Klopp, ambaye inadaiwa atasaini mkataba wa miaka mitatu.

Liverpool wanaamini Klopp, atakua muarobaini wa kumaliza tatizo la kusaka mafanikio klabuni hapo, ambalo limeduni kwa zaidi ya miaka kadhaa iliyopita, licha ya kuwa na wachezaji wenye hadhi kubwa duniani ambao walisajiliwa klabuni hapo chini ya utawala wa Rodgers.

Klopp, anajiandaa kurejea katika medani ya ufundishaji soka, baada ya kubatilisha msimamo wake wa kutaka kupumzika kwa muda wa msimu mazima, baada ya kuitumikia Borussia Dortmund kuanzia mwaka 2008–2015

Magufuli Amvaa Mbowe, Amuita Mzururaji
TFF Yasaini Kandarasi Ya Miaka Mitatu Na Star TV