Majogoo wa jiji Liverpool wapo katika hatari ya kupangwa kwenye kundi la kifo katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, kufuatia kutupwa katika chungu (Pot) cha tatu, baada ya klabu ya SL Benfica kufanikiwa kufuzu hatua ya makundi usiku wa kuamkia leo.
Endapo SL Benfica wangeshindwa kufuzu kwa hatua hiyo, zoezi la upangaji wa makundi litakalochukua nafasi mjini Monaco – Ufaransa leo jioni, lingekua rahisi kwa majogoo hao wa Anfiled, lakini uwepo wa timu hiyo kutoka Ureno, kunaifanya Liverpool kuangukia katika chungu (Pot) cha tatu, kinachowapeleka kwenye mtihani wa kupambana na timu nguli barani Ulaya.
SL Benfica waliichapa PAOK Salonika makabao 4-1 katika mchezo wa mkondo wa pili ulioungruma nchini Uguriki usiku wa kuamkia leo, baada ya matokeo ya sare ya bao moja kwa moja yaliyopatikana kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza, uliochezwa nchini Ureno juma lililopita.
Kwa mujibu wa kanuni za upangazi wa makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya SL Benfica ambao ni washindi wa pili katika ligi ya Ureno, wameangukia katika chungu (pot) cha pili, na kama wasingefuzu, nafasi yao ingechukuliwa na Liverpool ambao ndio kinara kwa kuwa na alama nyigi miongoni mwa timu zilizopo katika chungu (Pot) cha tatu.
Liverpool wana alama 62.000, tofauti ya alama mbili dhidi ya AS Roma wenye alama 64.000 katika viwango vya ubora wa soka upande wa klabu barani Ulaya.
Endapo Kikosi cha Jurgen Klopp kingeangukia katika chungu (Pot) cha pili kilikua na kila sababu za kuzikwenda klabu kama Borussia Dortmund, Porto, Shakhtar Donetsk, SL Benfica, SSC Napoli ama AS Roma, lakini kwa hali iliopo ni lazima Liverpool watapangwa na moja ya timu hizo .
Mgawanyo wa timu katika vyungu (pots) kuelekea zoezi la upangaji wa makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, litakalofanyika mjini Monaco-Ufaransa baadae hii leo.
Chungu (Pot) cha Kwanza.
Real Madrid, Atletico Madrid, FC Barcelona, Bayern Munich, Manchester City, Juventus, Paris Saint-Germain, Lokomotiv Moscow
Chungu (Pot) cha Pili.
Borussia Dortmund (89.000), Porto (86.000), Manchester United (82.000), Shakthar Donetsk (81.000), Benfica (80.000), Napoli (78.000), Tottenham (67.000), Roma (64.000)
Chungu (Pot) cha Tatu.
Liverpool (62.000), Schalke (62.000), Lyon (59.500), Monaco (57.000), Ajax (53.500), CSKA Moscow (45.000), Valencia (36.000), PSV Eindhoven (36.000)
Chungu (Pot) cha Nne.
Viktoria Plzen (33.000), Club Brugge (29.500), Galatasaray (29.500), Young Boys (20.500), Inter Milan (16.000), Hoffenheim (14.285), Red Star Belgrade (10.750), AEK Athens (10.000)
Muhimu: Namba zilziowekwa kwenye mabano ni alama (Point) ambazo zinazitofautisha klabu katika viwango vya soka barani Ulaya.