Klabu ya Liverpool inajiandaa kuwasilisha ofa ya Pauni 50 milioni kwa mara ya kwanza kwenda Southampton ili kuipata huduma ya kiungo wa timu hiyo iliyoshuka daraja msimu uliomalizika, Romeo Lavia.

Nyota huyu wa kimataifa wa Ubelgiji huduma yake pia inahitajika na Chelsea na Arsenal, lakini kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amewaambia mabosi wake kwamba anataka kumchezesha sambamba na Dominik Szoboszlai, hivyo wahakikishe anatua Anfield.

Liverpool ambayo ilikuwa na wakati mgumu katika msimu uliopita, wamiliki wake wamedhamiria kumpa n Klopp anachohitaji ili kuhakikisha kwamba timu inafanya vizuri katika mashindano mbalimbali itakayoshiriki msimu ujao, Lavia ni miongoni mwa mastaa waliofanya vizuri akiwa na Southampton licha ya timu hiyo kushuka daraja, ambapo amekuwa katika rada za timu mbalimbali huko England na Ulaya nzima kwa ujumla.

Licha ya Lavia mwenyewe amekwishaweka wazi kwamba anataka kuondoka katika kikosi hicho, lakini mabosi wa Southampton hawapo tayari kuona akiondoka kwa hasara na huenda wakahitaji zaidi ya Pauni 50 milioni.

Hata hivyo, mchezaji huyo amekuwa akishinikiza kuondoka na mabosi wamekuwa wakisisitiza pia kwamba hawapo tayari kuona akiondoka bila ya timu kupata chochote, kwani ni miongoni mwa mastaa wachache wenye ubora katika kikosi chao ambao wana uhakika wa kuuzika kwa bei nzuri.

Zoezi kura ya kutokuwa na imani na Rais kufanyika Julai 7
Mauzo Biblia kongwe Duniani yavunja rekodi