Majogoo wa Jiji ‘Liverpool’ wameripotiwa kuanza kuwasiliana tena na Borussia Dortmund kujadili uwezekano wa kumsajili kiungo Jude Bellingham kwenye dirisha la usajili majira ya kiangazi.

Liverpool, kuna wakati ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kumnasa Kiungo huyo wa kimataifa wa England kabla ya kujiweka pembeni kwa madai kwamba bei yake anayouzwa ni kubwa sana.

Real Madrid wakaonekana kuingia kwenye mpango wa kumchukua kiungo huyo wa zamani wa Birmingham City licha ya kwamba haikuwekwa wazi kama itakuwa tayari kulipa dau la Pauni 100 milioni linalotakiwa na Dortmund.

Kuna uwezekano mkubwa wa Bellingham akabaki Dortmund kwa msimu ujao wa 2023-24 ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kujumuishwa kwenye kikosi cha England kwa ajili ya Euro 2024.

Baada ya hapo, Bellingham atafikiria ishu ya kuhama na ndio maana Liverpool wanahitaji kunasa saini ya mchezaji huyo akakipige Anfield wakati wa dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi 2024.

Bellingham, 19, amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu, akifunga mabao 11 na kuasisti mara saba katika mechi 40 za michuano yote aliyotumika Dortmund.

Liverpool inataka kufanya mabadiliko makubwa kwenye sehemu yake ya kiungo baada ya wachezaji kibao wa eneo hilo akiwamo Naby Keita, Alex Oxlade-Chamberlain na James Milner wakijiandaa kuachana na maisha ya Anfield mwishoni mwa msimu huu.

Wafuasi wa Odero wafanya ibada nje ya Mahakama
Songo awania rekodi ya tatu Championship