Majogoo wa jijini Liverpool wameonyesha dhamira ya dhati ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa pembeni wa mashetani wekundu Man Utd, Ashley Simon Young ambaye kwa sasa hana nafasi kwenye kikosi cha Louis Van Gaal.

Liverpool, amejiandaa kumsajili mshambuliaji huyo kutoka nchini Uingereza kwa ada ya uhamisho wa paund million 8, ambayo wanaamini itatosha kutimiza lengo la kumtengenezea Young maisha mapya huko Anfield.

Liverpool wamejinasibu kuwa tayari kumlipa mshahara paund 118,000 kwa juma mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30.

Hata hivyo huenda majogoo wa jiji, wakapata upinzani mkali katika mipango ya usajili huo kufuatia uongozi wa klabu ya Tottenham Hotspurs kujipanga vilivyo kumuwani Young.

Lakini pamoja na kuwepo kwa taarifa za klabu hizo mbili kuwa tayari kumsajili Ashley Young, uongozi wa Man Utd pamoja na kumuweka sokoni mshambuliaji huyo, bado hawajathibitisha kufanya mazungunzo yoyote mpaka sasa.

Young amekua na wakati mgumu wa kumthibitishia meneja wa Man Utd, Louis van Gaal kama anaweza kucheza kila juma kutokana na changamoto iliopo kwa sasa kwenye kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria nchini  Uingereza.

Wasira Azungumzia Tuhuma Za Kumpiga Ngumi Mwenyekiti Wa CCM
Depay Atisha Mapokezi Ya Man Utd