Majogoo Wa Anfield wamaeshidwa kutamba wakiwa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na klabu ya Burnley katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliopigwa jana.

Burnley ndio walitangulia kupata bao dakika ya 27 kupitia kwa Scott Arfield kabla ya Mohamed Salah kusawazisha bao hilo dakika ya 30 na kufanya kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya 1-1.

Kikosi cha Liverpool kikiongozwa na Philippe Coutinho aliyerejea dimbani hapo jana kilizidi kufanya mashambulizi mengi kipindi cha pili lakini ilikuwa ngumu kuvunja ukuta wa ulinzi wa Burnley na kufanya dakiaka 90 kumalizika kwa sare ya 1-1.

Kwingineko klabu ya Tottenham ilijikuta ikishindwa kupata bao ikiwa katika uwanja wa nyumbani kwa mara ya kwanza katika michezo 30 baada ya kulazimishwa sare tasa na Swansea City.

Spurs walioichapa Bossia Dortmund mabao 3-1 katika mchezo wa ligi ya mabingwa wa Ulaya usiku wa Jumatano bado hawajashinda mchezo wowote wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu katika uwanja wa Wembey wanaoutumia kama uwanja wao wa nyumabani kwa muda.

Spurs walishidwa kufunga bao katika uwanja wa nyubani kwa mara ya kwanza kaika michezo 30

Kwa matokeo hayo Tottenham wapo katika nafasi ya 8 wakiwa wamecheza michezo minane wakati Liverpool nao wakiwa nafasi ya 8 baada ya kucheza michezo 5 wakitofautiana idadi ya magoli yan kufunga na kufungwa.

RC Gambo apiga marufuku viongozi kukamata watumishi
Nyumba yamtia matatani Zitto Kabwe