Majogoo wa jiji, Liverpool wamemtangaza rasmi Jurgen Klopp, kuwa mbadala wa meneja wa aliyetimuliwa klabuni hapo mwishoni mwa juma lililopita Brendan Rodgers.

Uongozi wa klabu ya Liverpool, ulimtangaza meneja huyo kutoka nchini Ujerumani kupitia kituo cha televisheni cha klabu hiyo (Liverpool TV) mishale ya saa nne usiku kwa saa za England ambapo kwa hapa nyumbani ilikua saa saba usiku.

Klopp, aliwasili mjini Liverpool jana mchana akitokea nyumbani kwao Mainz nchini Ujerumani, na alikua na mazungumzo ya mwisho na viongozi wa klabu ya Liverpool kabla ya kusaini mkataba wa kuanza kazi.

Hata hivyo kituo cha televisheni cha Sky Sport News, kilikua cha kwanza kuonyesha picha ambazo zilithibitisha safari ya meneja huyo akitokea nchini Ujerumani lakini watu hawakutilia maanani na waliamini huenda ilikua habari ya kupikwa.

Klopp, amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia klabu ya Liverpool, na mtihani wake wa kwanza utakua Oktoba 17, ambapo The Reds watakua na kibarua kigumu cha kuwakabili Tottenham Hotspurs kwenye uwanja wa Anfield.

Kwa mara ya mwisho meneja huyo mwenye umri wa miaka 48, alikua akiitumikia klabu ya Borussia Dortmund, na mwishoni mwa msimu wa 2014-15, alitangaza kuondoka klabuni hapo kwa kusudio la kuhitaji kupumzika.

Robert Lewandowski Achana Tiketi Ya Scotland
FA Watangaza Msimamo Wao Kwa Platini