Majogoo wa jiji Liverpool, wamekata rufaa ya kupinga adhabu ya mshambuliaji wao kutoka nchini Senegal Sadio Mane, baada ya kuonyesha kadi nyekundu wakati wa mchezo wa ligi ya nchini England dhidi ya Man City, uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita.

Mane alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kupiga teke mlinda mlango wa Man City Ederson sehemu za usoni na kumsababishia maumivu makali, ambayo yalimzuia kuendelea na mchezo huo, uliomalizika kwa majogoo wa jiji kufungwa mabao matano kwa sifuri.

Mshambuliaji huyo ambaye ni msaada mkubwa kwa Liverpool, alimuomba radhi Ederson kwa rafu mbaya aliyomchezea, kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook mara baada ya mchezo kumalizika katika uwanja wa Etihad huko mjini Manchester.

Mane aliandika: “Ninatarajia na kumtakia Ederson kupona kwa haraka.

“Niuwie radhi kwa kukuumiza sehemu za usoni, halikua kusudio langu kufanya vile, ila ilitokea kutokana na mazingira yaliyokuwepo kati yetu wakati tukiwania mpira. Ninarudia tena kwa kukutaka msahama na ninatarajia kukuona tena uwanjani siku za karibuni.”

Chama cha soka nchini England FA kinatarajia kusikiliza rufaa ya Liverpool hapo kesho.

Bony apambana na vijana wa Derby County
Mange asakwa na DCI, agubikwa na hofu