Michezo ya kuwania kufuzu kwenye mashindano ya Vilabu bingwa barani Ulaya yameanza hapo jana ambapo michezo kadhaa ilichezwa huku Klabu ya Liverpool kutoka Uingereza ikiibuka na ushindi wa magori 2-1 ugenini dhidi ya Hoffinhem ya nchini Ujerumani
Liverpool waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao hayo mawili kwa sifuri huku mabao ya Liverpool yakiwekwa kimiani na Alexandre Arnold dakika ya 35 na James Milner dakika ya 74 huku la Hoffeinheim likifungwa na Mark Uth dakika ya 87.
Aidha, michezo mingine iliyopigwa hapo jana kuwania kufuzu michuano hiyo ni pamoja na ule wa Klabu ya Sporting Cp ya nchini Ureno na FC FCSB ambao awalitoka suluhu ya bila kufungana na FC FCSB, huku CSKA Moscow nao wakatoka sare ya bila kufungana na Young Boys.
-
Mkongwe Wa Ligi Ya England Kuhamia The Hawthorns
-
Mabosi wa klabu za England kuwasilisha mapendekezo FA
-
Tim Krul akaribia mlango wa kutokea St James’ Park