Klabu ya Liverpool itakataa ofa yoyote ya Mohamed Salah, vyanzo vimeiambia ESPN, baada ya majaribio ya mabingwa wa Saudi Arabia, Al Ittihad kumfanya mshambuliaji huyo kuwa mchezaji wanayemwinda zaidi.

Salah mwenye umri wa miaka 31 ameonekana kulengwa na Al Ittihad, ambao wanamtaka mchezaji huyo wa kimnataifa wa Misri kuunda ushirikiano na mshabuliaji wa zamani wa Real Madrid, Karim Benzema katika timu hiyo yenye maskani yake katika jiji la Jeddah.

Fabinho, mchezaji mwenzake wa zamani wa Liverpool, aliondoka na kwenda Al Ittihad kwa ada ya pauni milioni 40 mwezi uliopita, vyanzo vimeiambia ESPN klabu hiyo ya Saudi iko tayari kulipa ada kubwa na mshahara mnono ili kumsajili Salah, ambaye alisaini mkataba mpya wa miaka mitatu pale Anfield mwaka jana.

Lakini licha ya uwezekano wa Liverpool kumwekea Salah ada kubwa kwa kumruhusu mchezaji huyo kuondoka, vyanzo vimesema klabu hiyo haina nia ya kuachana na nyota huyo.

Liverpool inafahamu nia ya Al Ittihad, lakini bado haijapokea ofa yoyote rasmi au isiyo rasmi kutoka kwa klabu hiyo, lakini ofa kwa Salah itakataliwa.

Ingawa dirisha la usajili la majira ya joto linafungwa Septemba Mosi, dirisha la uhamisho la Saudi Arabia limesalia wazi hadi Septemba 20, na kuziwezesha timu zake kusajili wachezaji kutoka Ulaya kwa majuma matatu zaidi baada ya dirisha lao kufungwa.

Mapema mwezi huu, Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alitoa wito kwa FIFA na UEFA “kutafuta suluhisho” juu ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho la Saudi Arabia mapema.

Ndege ya Rais haijazuiliwa Dubai, ni uzushi - Simbachawene
Serikali kuendeleza uungaji mkono Vijana wabunifu