Kiungo kutoka nchini Brazil Fábio Henrique Tavares ‘Fabinho’ ameachwa katika kikosi cha Liverpool ambacho kipo Singapore kwa ajili ya ziara ya maandalizi ya msimu mpya wa 2023.
Kwa mujibu wa ripoti Mbrazili huyo anakaribia kuungana na Jordan Henderson ambaye amekamilisha uhamisho wa kujiunga na Al-Ettifaq kutoka Saudi Arabia.
Fabinho atakosa mechi za kirafiki ambazo zitachezwa Singapore dhidi ya Leicester City na Bayern Munich.
Kiungo huyo wa zamani wa Monaco ambaye aliyejiunga na Liverpool mwaka 2018 alikuwa sehemu ya mafanikio ya klabu hiyo ilipobeba ubingwa wa Ligi Mabingwa Ulaya na Ligi kuu England.
Sasa kwa mujibu wa ripoti huenda akajiunga na Al-Ittihad siku chache zijazo kwani bado nyaraka kadhaa tu za kusainiwa.
Liverpool inatarajia kupokea Pauni 40 milioni kwaajili ya Fabinho baada ya kumuuza Henderson kwa Pauni 13 milioni.
Mipango ya Liverpool baada ya kumuuza Fabinho ni kufukuzia saini ya kiungo wa Souhampton Romeo Lavia miaka 19.
Imeelezwa kwamba Liverpool na Southampton zinatarajia dili hilo litakamilika haraka iwezekanavyo kabla ya msimu mpya kuanza.
Kuondoka kwa Henderson na Fabiho itabadilisha sura ya safu ya kiungo ya Liverpool baada ya viungo wengine kama James Milner, Naby Keia na Alex Oxlade-Chamberlain kuondoka.