Uongozi wa klabu ya Liverpool, una matumaini ya kumalizana na aliyekua meneja wa klabu ya Borussia Dortmund, Jurgen Klopp baada ya kuthibitisha kumfuta kazi Brendan Rodgers mwishoni mwa juma lililopita mara baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Everton.

Liverpool wana matumaini ya kukamilisha mpango wa kumuajiri Klopp hadi itakapofika siku ua ijumaa, kufuatia taratibu za mazungumzo kwenda vyema tangu jana.

Mazungumzo kati ya uongozi wa Liverpool na muwakilishi wa Klopp yameonyesha matumaini makubwa ya kupatikana kwa muafaka wa pande hizo mbili kufanya kazi kwa pamoja kutokana na hitaji la meneja lililopo huko Anfield kwa sasa.

Klopp mwenye miaka 48, raia wa Ujerumani, ameshatangaza rasmi kuwa tayari kufanya kazi na klabu yoyote kwa sasa, baada ya kuonyesha msimamo wake wa kuhitaji kupumzika sambamba na kuikataa shughuli ya kwenda nchini Mexico ambapo aliombwa kuwa mrithi wa Miguel Herrera, katika timu ya taifa ya nchi hiyo.

Endapo Klopp, atafanikisha mpango wa kuelekea mjini Liverpool, kibarua chake cha kwanza kitakuwa dhidi ya Tottenham Hotspurs ambao watafunga safari kuelekea Anfield, oktoba 17.

David Moyes Akataa Kurejea England
Mwenyekiti Chama Cha Walimu Chato Aliyepanda Jukwaani La Lowassa Ashtakiwa