Uongozi wa klabu ya Liverpool umethibitisha rasmi kuwa kiungo mshambuliaji kutoka nchini Brazil, Roberto Firmino Barbosa de Oliveira atavaa jezi namba 11.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, alisajiliwa na majigoo wa jiji mwezi uliopita akitokea nchini Ujerumani alipokua akiitumikia klabu ya Hoffenheim, na uthibitisho wa matumizi ya jezi namba 11 umedhihirisha mmiliki wa namba hiyo Oussama Assaidi atatafutiwa namba nyingine.

Naye mshambuliaji wa pembeni, James Milner ambaye amejiunga na klabu ya Liverpool kama mchezaji huru baada ya kukamilisha mkataba wake na Man City, amekabidhiwa jezi namba saba ambayo kwa mara ya mwisho ilikua ikitumiwa na mshambuliaji kutoka nchini Uruguay, Luis Suarez ambaye aliondoka klabuni hapo mwaka jana na kujiunga na FC Barcelona.

Jezi namba saba huko Anfield imekuwa na historia nzuri ndani ya kikosi cha Liverpool baada ya kutumikiwa na magwiji wa klabu hiyo King Kenny Dalglish pamoja na Kevin Keegan.

Kwa upande wa beki wa kulia ambaye amesajiliwa na Liverpool akitokea Southampton, Nathaniel Clyne atavaa jezi namba mbili iliyowahi kutumiwa na Glen Johnson, huku Danny Ings aliyesajiliwa akitokea Bunrley amekabidhiwa jezi namba 28.

Kiungo na nahodha wa sasa wa Liverpool Jordan Henderson naye amepewa heshima ya kurithi jezi namba nane iliyokua inatumiwa na aliyekua nahodha na kiungo klabuni hapo Steven Gerrard, ambaye ametimkia nchini Marekani na kujiunga na klabu ya Los Angles Galaxy.

Southampton Yampata Mrithi Wa Schneiderlin
Jeremain Lens Kufanya Tena Kazi Na Advocaat