Nchini Uingereza michuano ya Carabao Cup imeanza vibaya kwa majogoo wa London Liverpool baada ya kukubali kipigo kutoka kwa Leicester City katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa King Power.

Mshambuliaji Shinji Okazaki alitangulia kuipatia Leicester City katika dakika ya 65 likiwa ni bao lake la nne kuifungia Leicester msimu huu kabla ya Islam Slimani kupachika bao la pili kwa shuti kali na kuiondosha Liverpool katika michuano ya Carabao Cup kwa ushindi wa 2-0.

Kwingineko bao pekee lililofungwa na Delle Ali limeifanya Tottenham kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burnley  huku Swansea City wakipata ushindi wa mabao 2 ugenini dhidi ya Reading.

Michuano hiyo itaendelea leo katika raundi ya tatu ambapo michezo michezo mitano itapigwa leo katika viwanja tofauti.

Arsenal watacheza dhidi ya Doncaster, Chelsea watacheza na Nottingham Forest,Everton dhidi ya Sunderland, Manchester United dhidi ya Burton Albion wakati West Bromwich watakipiga didi ya Man City.

 

Video: Miili 13 ajali ya Uganda kuzikwa mikoa mitatu, Vigogo CCM waanza kukimbia uchaguzi
Burundi yataka wapenzi kuoana kilazima, yatoa muda