Klabu ya Crystal Palace imetangaza kumsajili kwa mkopo mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa Loic Remy akitokea magharibi mwa jijini London yalipo makao makuu ya Chelsea.

Crystal Palace wametangaza kumsajili mshambuliaji huyo hadi mwishoni mwa msimu huu, huku faida iliyowanufaisha imetokana na Remy kutokuwepo kwenye mipango ya meneja mpya wa Chelsea Antonuio Conte katika kipindi hiki cha msimu wa 2016/17.

Klabu hiyo ya jijini London imethibitisha usajili wa Remy kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter: “#CPFC inayofuraha kutangaza usajili wa Loic Remy akitokea @ChelseaFC kwa mkopo wa muda mrefu.”

Chelsea nao wameandika katika tovuti yao kuwa: “Loic Remy ataitumikia Crystal Palace kwa msimu mzima wa 2016-17.

Remy amesaliwa na mkataba wa miaka miwiwli wa kuendelea kutumikia klabu ya Chelsea.

Video: Mo Dewji amhakikishia Waziri Mkuu kuiunga mkono Serikali, Atangaza kuwekeza zaidi
Simba SC Yaitikia Agizo La Rais Magufuli Kwa Vitendo