Mlinda mlango wa klabu ya Liverpool, Loris Karius huenda akatimkia nchini Italia katika klabu inayoshiriki ligi daraja la tatu baada ya kuboronga kwenye fainali ya ligi ya mabigwa Ulaya.
Rais wa klabu ya Rimini FC inayocheza ligi ya daraja la tatu nchini Italia amesema yuko tayari kumchukua mlinda lango huyo kwa mkopo wa mwaka mzima.
Tarehe 22 mwezi Juni mwaka huu itakuwa ni siku ya kuzaliwa ya Loris Karius anayetimiza umri wa miaka 25 na rais wa klabu ya Rimini FC amesema atamsajili kama zawadi yake ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ili mjerumani huyo aweze walau kutulia na kujiamini tena.
Karius alifanya makosa katika mchezo wa fainali ya klabu bingwa barani Ulaya na kupelekea Liverpool kufungwa na Real Madrid mabao 3-1.