Real Madrid itacheza hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Juventus FC, baada ya kupata ushindi wa jumla wa mabao manne kwa mawili dhidi ya Atletico Madrid.

Real Madrid walicheza ugenini Vicente Calderon usiku wa kuamkia leo, walikubali kufungwa mabao mawili kwa moja, lakini ushindi wa mabao matatu kwa sifuri waliouvuna kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza yaliwasaidia kufanikisha safari ya kucheza hatua ya fainali.

Katika mchezo jana uliochezeshwa na Mwamuzi, Cuneyt Cakir kutoka nchini Uturuki, ilishuhudiwa wenyeji Atletico Madrid wakijipatia mabao yao mwanzoni mwa kipindi cha kwanza katika dakika za 11 na 15 kupitia kwa Saul Niguez na Antoine

Griezmann alifunga kwa mkwaju wa penati baada ya Fernando Torres kuangushwa ndani ya boksi na Rafael Varane. Bao la Real Madrid likafungwa na Fransesco Isco Alcaron katika dakika ya 42.

Hatua ya fainali ya klabu bingwa barani Ulaya safari hii itachezwa Jumamosi ya Juni 3 nchini Wales kwenye dimba la Millenium mjini Cardiff.

Endapo Real Madrid watatwaa ubingwa wa Ulaya mbele ya Juventus FC (Vecchia Signora) wataweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuutwaa ubingwa huo mara mbili mfululizo. Real Madrid ndiyo mabingwa watetezi.

Man Utd Yarudi Mtaa Wa Sita, Arsenal Ikishinda St. Mary's
Majaliwa azungumzia hali ya sukari nchini