Meneja wa klabu ya Man Utd, Louis Van Gaal amesema amechoshwa na baadhi ya mechi za timu yake msimu huu.

”Kuna mechi ambazo hata mie nimezifurahia”,alisema raia huyo wa Uholanzi.Na pia kuna mechi ambazo zinachosha na kunikasirisha kwa sababu tunashindwa kupita safu ya nyuma ya upinzani, lakini hiyo ni soka”.

Timu hiyo ya Van Gaal ilizomewa wakati wa mapumziko wakati wa mchezo wa kombe la FA mwishoni mwa juma lililopita, ambapo timu hiyo ilichomoza na ushindi dhidi ya Shiffield United 1-0, huku maelfu ya wafuasi wakiondoka mapema uwanjani.

Akiulizwa ni kwa nini mashabiki wengi waliondoka mapema kabla ya Wayne Rooney kufunga kwa njia ya mkwaju wa penati, katika dakika ya 93,Van Gaal alijibu,”Hawafikirii kwamba tutafunga na pengine ni kwa sababu mashabiki ni wengi mno”.

Ratiba Mzunguuko Wa Tatu Kombe La FA Yatolewa
UVCCM wataka CCM imfukuze Amani Karume