Aliyekua meneja wa klabu ya Man Utd, Louis van Gaal ni miongoni mwa mameneja wanaopewa kipaumbele cha kukabidhiwa kikosi cha klabu ya AC Milan ya nchini Italia ambacho kwa sasa hakina mkuu wa benchi la ufundi baada ya kutimiliwa kwa Sinisa Mihajlovic mwishoni mwa msimu uliopita.

Van Gaal ambaye aliondoka Man Utd, siku chache baada ya kuiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa kombe la FA nchini Engalnd mwezi uliopita, amekuwa sehemu ya orodha ya watu hao, kutokana na uzoefu alionao katika medani ya ufundishaji soka la barani Ulaya.

Uongozi wa AC Milan umelazimika kuendelea na mchakato wa kumsaka meneja wa kikosi chao, baada ya mazungumzo kati yao na aliyekua meneja wa klabu ya Man City, Manuel Pellegrini kuingia dosari.

Hata hivyo yapo majina ya mameneja wengine ambao watawania nafasi ya kukabidhiwa benchi la ufundi la klabu hiyo kongwe nchini Italia pamoja na mjini Milan.

Miongoni mwa mameneja hao ni Frank de Boer , Andre Villas-Boas, Rudi Garcia pamoja na Laurent Blanc.

Uongozi wa klabu ya AC Milan umekua katika hatua ya kumsaka meneja mwenye vigezo vya hali ya juu, kutokana na kuhitaji kuona kikosi chao kikirejea kwenye ushindani wa soka la barani Ulaya, hususan kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani humo, ambayo kwa mara ya mwisho walionekana mwaka 2013.

Meneja mpya wa FC Bayern Munich, Carlo Ancelotti anaendelea kukumbukwa klabuni hapo, kufuatia mazuri aliyoyafanya na kuiwezesha The Rossoneri kutwaa ubingwa wa barani Ulaya mwaka 2003 pamoja na 2007.

AC Milan ni moja ya klabu iliyowahi kutwaa mara nyingi ubingwa wa barani Ulaya ambapo mpaka sasa wameshafanya hivyo mara saba, ikitanguliwa na Real Madrid waliotwaa ubingwa mara 11 huku nafasi ya tatu ikishikwa na FC Bayern Minich waliotwaa ubingwa mara tano.

Nisha kufturu pamoja na watoto waishio kwenye mazingira magumu Dar.
Mikel Arteta Kumsaidia Pep Guardiola Man City