Waziri Mkuu Mstaafu, Mbunge wa jimbo la Monduli, Edward Lowasa amewataka watu wanaeneza habari kuwa yeye ni mla rushwa na fisadi wajitokeze hadharani na kutoa ushahidi kwa kuwa tuhuma hizo hazina ukweli wowote.

Lowasa ametoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kurejesha fomu za kuwania kuchaguliwa na Chama Cha Mapinduzi kugombea nafasi ya Urais, katika ofisi za makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma.

“Maneno hayo sasa basi, natoa changamoto kwa yeyote mwenye ushahidi huo autoe hadharani vinginevyo waache kueneza uvumi na uongo,” alisema Lowasa na kuongeza kuwa mtu huyo atoe ushahidi wa siku, saa na mtu aliyempa rushwa.

Alisisitiza kuwa yeye kiongozi safi na endapo atapata nafasi ya kuingia ikulu atawapinga wala rushwa na kuchukua hatua sitahiki bila kumuonea mtu na ataiendesha nchi kwa kuheshimu katiba ya nchi.

Jana watia nia zaidi 32 waliwasilisha fomu baada ya kupata wadhamini katika mikoa mbalimbali ya nchi huku mlango ukitarajiwa kufungwa leo (July 2, 2015).

Van Parsie Kuwa Mbadala Wa Demba Ba, Ligi Ya Uturuki
'Nusu Nusu' ya Joh Makini yashika Namba 1 Chart ya MTV Base