Zikiwa zimebaki siku 31 kabla watanzania hawajapiga kura kumchagua rais, Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa ambaye amekuwa akieleza imani yake kuwa atashinda kwa kishindo, ameeleza msimamo wake endapo tume ya Taifa ya Uchaguzi itangaza matokeo tofauti na matarajio yake.

AKiongea na kituo cha Runinga cha ‘Citizen’ cha nchini Kenya, Lowassa amesema hawezi kusema kama atakubali au atakataa hadi itakapothibitika kuwa matokeo hayo hayajahujumiwa.

“Siwezi kusema nitaichukulia kama nimeshindwa hadi nitakapothibitishiwa kuwa kila kitu kimeenda sawa na taratibu na kama hakuna hujuma,” alisema. “Tunaogopa sana kuhusu hujuma, kila mtu unaeongea nae unapokutana nae anakwambia ‘utashinda, lakini je, watakubali kushindwa?” Aliongeza.

Katika hatua nyingine, Lowassa alijibu swali la mwandishi lililomtaka kueleza kama angeweza kusema anachokisema hivi sasa kuhusu CCM endapo angechaguliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCCM.

“Ninasema vitu vingi ambavyo vingeweza kufanywa vizuri zaidi na CCM, na ninasema vitu vingi ambavyo ninaweza kuvifanya nikiwa katika upinzani zaidi ya ambavyo ningekuwa CCM,”alieleza waziri Mkuu huyo mstaafu.

Picha: Lowassa Atikisa Kwa Nape, Maelfu Warudisha Kadi Za CCM
Twiga Stars Kujipima Kwa Malawi