Wakati ambapo wananchi wana kiu ya kufahamu Ukawa watafanya lini uzinduzi wa kampeni zao hasa kwa kuzingatia kuwa CCM imefanya uzinduzi wa kishindo jana katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam, mgombea urais wa Chadema na Ukawa, Edward Lowassa ameanza ziara ya kupanda usafiri wa umma (daladala).

Lowassa ameanza ziara yake asubuhi hii ambapo anapanda katika usafiri huo wa umma kwa lengo la kuwafikia wananchi wa maisha ya chini kabisa ili awasikilize kwa ukaribu na kufahamu kero zao.

Katika baadhi ya picha zinazoonekana, Lowassa anaonekana akiwa katikati ya daladala ikitokea Gongo la Mboto kuelekea Chanika jijini Dar es Salaam. Chanika ni eneo ambalo liko pembeni kabisa ya jiji la Dar es Salaam na ni moja kati ya sehemu ambazo wananchi wa eneo hilo wanakumbwa na uhaba wa huduma ya usafiri.

Bolt Adhihirisha Ubora Wake Mjini Beijing
Mwinyi Aivuruga Ukawa, Kauli za Mkapa Zawapa Ukawa 'Point' Ya Kuanzia