Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyamavya vya upinzani vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa ameendelea kusisitiza kipaumbele cha elimu katika serikali yake na wakati huu ametoa habari njema kwa wote waliowahi kusoma vyuo vikuu na wanadaiwa na Bodi ya Mikopo.

Akiwa wilayani Same, Kilimanjaro hivi karibuni, katika moja kati ya mikutano yake ya kampeni, Lowassa alisema kuwa pamoja na kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu, serikali yake itasamehe mikopo ya wale wote wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).

“Serikali yangu itatoa elimu kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu bure na wanaodaiwa na Bodi tutawafutia mikopo yao,” alisema na kushangiliwa na wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.

Aidha, Lowassa aliwaahidi wakazi wa Same kuwa endapo ataingia madarakani, atahakikisha analimaliza tatizo la maji wilayani hapo kwa asilimia 100.

 

Rihanna Mabusu Tele Na Kijana Huyu Mdogo
Umoja Wa Mataifa Waelezea Picha Ya Ushindi Uchaguzi Mkuu