Macho ya wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa hususani kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu, jana yalielekezwa Chato na kushuhudia mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa akipata mapokezi makubwa katika jimbo hilo linakaliwa na mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli.

1

Akiwa katika jimbo hilo, Lowassa alipokea malalamiko kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani humo, Lucas Michael.

Bw. Michael alimkosoa vikali Dk. John Magufuli kwa madai kuwa ingawa amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka mingi, ameshindwa kutetea maslahi ya walimu. Alidai kuwa walimu wanafikia hatua ya kujinunulia wenyewe chaki za kufundishia na kwamba halmashauri ya wilaya hiyo haiwalipi hata fedha za safari pamoja na kukataa kuwaendeleza kielimu.

2

Mwenyekiti huyo aliikosoa kauli ya Dk Magufuli kuwa watanzania wamchague kwa kuangalia mfano wa maendeleo aliyoyaleta katika jimbo lake la Chato.

“Namuuliza Dk Magufuli mbona katika halmashauri yake haisomeshi wafanyakazi, mbona wakistaafu hawapewi fedha za kusafiri kuelekea makwao, mbona wanajinunulia chaki wenyewe,” alihoji.

4

Lowassa aliahidi kutatua kero za walimu katika jimbo hilo pamoja na kufufua viwanda vilivyomo mkoani humo. Baada ya kuelezwa kuhusu kero ya maji inayowakabili wananchi wa eneo hilo, aliahidi kuitatua kwa kuvuta maji kutoka ziwa Victoria.

8

9

10

Shabiki Nguli Wa Brazil Afariki Dunia
CCM Wanamtaka Lowassa...