Wakati wananchi wakiendelea kufuatilia kwa ukaribu kampeni za urais, ubunge na udiwani, mgombea urais kwa tiketi ya Chadema amewataka wananchi kujipima wenyewe kama bado wanahitaji kuongozwa na serikali ya CCM.

Akihutubia umati mkubwa wa uliojitokeza katika viwanja vya polisi katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Lowassa aliwaambia wananchi hao kujipima kama wanahitaji bado maisha ya shida chini ya serikali ileile ya CCM au wanahitaji maisha bora kwa kufanya mabadiliko.

“Jipimeni kama bado mnahitaji mmlo mmoja, milo miwili au mnataka milo mitatu,” alisema.

Lowassa ambaye alitua Nzega kwa kutumia chopa alifanya mikutano minne katika mkoa wa huo akiwahimiza wananchi kumchagua yeye na wagombea wa vyama vinavyounda Ukawa kwa kuwa watawaletea maendeleo na kubadilisha maisha yao.

Lowassa anaendelea na kampeni za urais katika maeneo mbalimbali nchini ambapo leo anatarajia kutua jijini Dar es Salaam na kufanya kampeni katika majimbo ya uchaguzi ya jiji hilo.

De Gea Ajitokeza Mtandaoni Baada Ya Juma Moja
Iceland, England, Czech Republic Zatangulia Ufaransa