Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa ambaye hivi karibuni alipigwa marufuku kufanya ziara za kushtukiza katika maeneo mbalimbali Dar es Salaam, amekuja na mbinu mpya ya kampeni kwa wanawake.

Leo (Agosti 27), Lowassa anatarajia kukutana na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya wanawake katika ukumbi wa Millennium Tower, jijini Dar es Salaam ambapo atazungumza mikakati aliyonayo katika kuwasaidia wanawake nchini endapo atachaguliwa kuwa rais.

Katika mkutano huo utakaorushwa moja kwa moja na kituo cha ITV na Azam TV kuanzia majira ya saa nane mchana, mke wa mgombea huyo wa urais Bi. Regina Lowassa pamoja na mke wa mgombea mwenza watazungumza na wanawake hao.

“Kesho Agosti 27, mheshimiwa Lowassa atazungumza na wanawake wa Tanzania. Atazungumza na wanawake wa Tanzania kwa maana kwamba kuna wanawake wa makundi mbalimbali ambao tumewaalika, lakini pia kwa taarifa hii ya BAWACHA, milango iko wazi kwa mwanamke yeyote Yule wa Tanzania ambaye anaishi Dar es Salaam na anataka kwenda kumuona Mheshimiwa Lowassa akitoa maono yake,” alisema Kiongozi wa BAWACHA, Halima Mdee.

Lowassa anaongea na makundi hayo wakati akitarajiwa kuzindua rasmi kampeni za Ukawa, Agosti 29 jijini Dar es Salaam.

‘Helkopta’ Rukhsa Kunogesha Kampeni
Mbatia Amtaka Kova Amkamate Mkapa