Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa ametangaza neema kwa wenyeviti wa serikali za mitaa ikiwa ni pamoja na wenyeviti wa vijiji na wenyeviti wa vitongoji endapo atachaguliwa kuwa rais wa Tanzania.

Akiongea kwa nyakati tofuati jana na juzi katika mikutano ya kampeni, Lowassa amesema kuwa serikali yake itahakikikisha inatoa posho ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na usalama katika maeneo yao.

Naye waziri Mkuu wa Mstaafu, Frederick Sumaye ambaye alikuwa katika jimbo alilolitumikia kwa miaka 20 kama mbunge, alitumia muda huo kutoa elimu kwa wananchi wa jimbo hilo kuwa wanapaswa kuangalia mgombea urais wa Chadema kwenye karatasi za kupigia kura na kwamba wasifikirie kuwa watakuta ‘Ukawa’ kwenye karatasi hizo.

“Kwa upande wa urais, tunamchagua ndugu yetu Lowassa ambaye atakuwa wa tiketi ya Chadema, sio tiketi ya Ukawa, usitafute Ukawa, ni Chadema,” Sumaye alifafanua.

Katika hatua nyingine, akiwa katika jimbo la Hanang, Lowassa alitoa mkono wa pongezi kwa mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kwa uamuzi wake wa kukitosa rasmi Chama Cha Mapinduzi (CCM), alichokitumikia kwa muda mrefu. Hata hivyo, Lowassa hakuingia ndani katika kuelezea pongezi zake.

Mzee Kingunge, jana alitangaza kuachana rasmi na CCM kwa madai kuwa viongozi wa chama hicho wamekiuka katiba ya chama na kwamba chama kimekosa muelekeo sahihi.

Magufuli: Nitaunda Serikali Ya Huduma Za Papo Kwa Papo
Mpango Wa Dk. Slaa Dhidi La Lowassa Na Ukawa Sasa Hadharani