Wakati kampeni za uchaguzi mkuu zikiendelea, mgombea urais kupitia Chadema anaeungwa mkonona vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa ameendelea kutaja idadi ya kura anazohitaji ili kujihakikishia ushindi ambapo jana aliongeza idadi.

Akiongea jana na maelfu ya wananchi wa Bariadi mkoani Simiyu, Lowassa ambaye amekuwa akisema anahitaji kura miloni 11, aliwaambia wananchi hao kuwa anahitaji kura milioni 13 hivyo anaomba wampigie kura na kuwashawishi watu wao wa karibu kufanya hivyo pia ili kuhakikisha anafikia kiwango hicho.

Lowassa aliwasisitiza wananchi hao kuwa idadi hiyo ya kura itamhakikishia ushindi dhidi ya CCM ambao alidai wananjama za kumuibia kura hizo.

“Sina maneno mengi ninayoweza kuwashukuru, nawaomba kura nyingi na za kutosha kwa sababu nahitaji zaidi ya kura milioni 13 ili kuwashinda hawa [CCM], si mnajua wanaweza kuiba, mnipige kura nyingi ili hata wakiiba zitoshe,” alisema.

Kadhalika, Lowassa aliahidi kuinua kilimo cha Bariadi kupitia kipaumbele chake cha elimu kwa kuwa bila elimu ya kilimo bora na cha kisasa, wakulima hawawezi kufanikisha lengo lao la kujikomboa kiuchumi.

Alisema elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu inawezekana na kwamba hiyo itasaidia kuwakomboa wakulima kwa kuzalisha wataalamu wengi zaidi katika sekta hiyo.

 

Polisi Wamsaka ‘Daudi Balali’ Twitter
Magufuli Awaonya Wakimbizi Wanaoingia Na Silaha Nchini