Edward Lowassa, ameahidi mbinu mpya atakayotumia ya kupambana na rushwa endapo atachaguliwa kuwa rais wa serikali ya awamu ya tano, mbinu ambayo amesema itaanza kufanya kazi siku 100 tu baada ya yeye kuingia madarakani.

Akiongea katika mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika Hai, Lowassa alieleza kuwa ataunda vituo maalum vitakavyokuwa vikitoa huduma za serikali katika kila wilaya, vituo hivyo vitarahisisha kupatikana kwa huduma za serikali na kuondoa urasimu nchini uliobainika kuwa chanzo kikubwa cha rushwa.

“Eneo la rushwa linawapa tabu sana serikali, lakini nitafanya utaratibu siku 100 za serikali yangu, tutaunda chombo kwenye kila wilaya, ukienda mjini kufata huduma za kiserikali unapata katika kituo kilekile. Inakuwa one stop center, inaondoa urasimu inaondoa mianya ya rushwa,” alisema Lowassa.

Akifafanua jinsi mbinu hiyo itakavyotumika, alisema kama mtu anataka kupata huduma kama leseni ya biashara atakuwa na uwezo wa kuipata katika kituo hicho kwa kufuata taratibu wa biashara unafuatwa.

CCM: Ikulu Hapahitaji Mtunisha Misuli au Tyson
Magufuli Azua Taharuki, Achanganya Majina Ya Wasaliti Na Watiifu