Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana alivunja rekodi ya kuwa mwanasiasa aliyewahi kushika nyadhifa ya juu zaidi Serikalini tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, kushikiliwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi.

Lowassa alikuwa miongozi mwa viongozi wa ngazi za juu wa Chadema ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu waliohojiwa jana kwa saa tatu ndani ya kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao wa Chadema walifika katika kituo hicho baada ya polisi kuvamia mkutano wa ndani waliokuwa wakiufanya katika hotel ya Giraffe view jijini humo na kuwataka kuvunja mkutano huo kwakuwa ulikuwa unakiuka katazo la Jeshi la Polisi kuhusu kutofanyika kwa mikutano yote ya ndani na nje ya vyama vya siasa.

Mkutano huo uliokuwa na wajumbe 178, pia uliwahusisha wabunge wa Chadema pamoja na baadhi ya madiwani na viongozi wengine wa chama.

“Mbowe aligoma na kusema kuwa wao wapi kisheria ndani ya ukumbi, ndipo wale polisi wanane walioingia ndani ya ukumbi huo walipowataka viongozi wote kutii sheria na waende wenyewe Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati,” alisema mmoja wa viongozi wa Chadema aliyekuwa ndani ya mkutano huo.

Viongozi hao wote waliwasili katika kituo hicho cha polisi majira ya saa 10 jioni na kuhojiwa hadi saa 1 usiku, kisha kuachiwa kwa dhamana.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema kuwa viongozi hao ikiwa ni pamoja na Lowassa na Mbowe wanahojiwa kuhusu kuandaa maandamano ya UKUTA, Septemba 1 pamoja na kufanya mikutano ya ndani iliyozuiwa.

“Tunawashikilia viongzoi kadhaa wa Chadema akiwemo Lowassa na Mbowe na kubwa tunataka kujua kikao chao wamefanya kwa sababu gani hali ya kuwa vimepigwa marufuku lakini wao wameendelea kufanya,” Kamanda Sirro anakaririwa na Mtanzania.

“Pia, tunataka kujua kwanini wanahamasisha maandamao wakati tayapelekea uvunjifu wa amani,” aliongeza.

Hata hivyo, Mwanasheria wa Chadema, Tundua Lissu aliyefika kituo hapo na kuzuiwa kuingia ndani, alisema kuwa kitendo hicho ni uonevu kwani mikutano ya ndani ya chama iko kikatiba na kusisitiza kuwa hawataka kata tamaa kudai kile walichodai kuminywa kwa demokrasia nchini.

Lipumba amvaa Maalim Seif,adai ana ‘Udikteta’, amkana Mtatiro
Lipumba Aendelea Kung'ang'ania Uenyekiti Wake CUF