Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amewataka viongozi wa CCM kuacha kumzushia na kusema uongo bali wajikite katika kujibu hoja zitakazowaletea maendeleo wananchi.

Lowassa aliyasema hayo jana mjini Dodoma katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika eneo uwanja wa Kibaigwa Makaburini.

Pamoja na mambo mengine, mgombea huyo anaewakilisha vyama vinavyounda Ukawa, alisema amekuwa akizushiwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na taarifa kuwa anamiliki wa eneo kubwa la ardhi liliko katika eneo la Lutangosi katika mpaka wa Kiteto na Kongwa, Dodoma.

“Nataka niwahakikishie, sina ardhi huku na mimi si mwendawazimu, kwa hiyo anayesambaza uongo huo aache au akachukue hilo eneo liwe mali yake. Nawatahadharisha waache kusema uongo kuwapotosha wananchi kwa matusi kwani hayanasaidii chochote, wajibu hoja za maendeleo kwa sababu ya ya kitu wanachotaka kukifanya,” alisema.

Kadhalika, Lowassa anayeongozwa na kauli mbiu ya ‘Mabadiliko’ katika kampeni zake, alisema kuwa endapo atachaguliwa kuwa rais wa Serikali ya awamu ya tano, atafuatilia madeni ya nje ya Tanzania ambayo yanapelekea kila raia kudaiwa wastani wa shilingi laki nane.

Alisema atafanya ufuatiliaji ili kubaini fedha hizo zilitumika kufanya nini ili kubaini kama kuna fedha zilizotumika kwa kufanya ziara pekee. aliwataka wahusika kuandaa maelezo juu ya suala hilo kwani watakapoingia Ikulu watayahitaji.

“Nasema waache kupiga kelele nyingi, watutayarishie maelezo tu, maana lazima ikulu tutaingia tu watake wasitake, tuatawataka vilevile wajibu hoja,” Lowassa aliongeza.

 

 

Palestina Kupeperusha Bendera Ofisi Za UN, Israel Yapinga
Chup* Ya Gwajima Yatinga Mahakamani Kama Ushahidi