Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amefafanua kuhusu operesheni iliyopewa jina la UKUTA akidai ni zoezi tofauti na linavyotafsiriwa na baadhi ya watu.

Akizungumza jana mjini Tunduma katika kikao cha ndani cha chama hicho, Lowassa alisema kuwa UKUTA sio oparesheni iliyolenga kufanya fujo au kuleta machafuko nchini bali imelenga katika kudai haki ya kidemokrasia aliyodai inaminywa.

Lowassa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani aliongeza kuwa hawana nia ya kupambana na Polisi ambao ni ndugu zao na watanzania wenzao.

“Hivi Chadema ni nani wakapambane napolisi ambao ni watoto wetu, ndugu zetu na hata wake na waume zetu? Alihoji Lowassa.

“Ila tunawahakikishia hatutorudi nyuma pale katiba na haki ya kidemokrasia itakapochezewa au kuwa chini ya mtu fulani. Najua Polisi watapiga watu, wataumiza watu na hata kuua, lakini niwahakikishie tu wao na walio  na Mamlaka wataishia katika mahakama ya Kimataifa,” alisema Lowassa.

Hata hivyo, Lowassa alisisitiza kuwa milango iko wazi bado kwa ajili ya mazungumzo ya kusaka muafaka kati ya pande zote ili kuepusha hali iliyopo.

Jeshi la Polisi limepiga marufuku kufanyika kwa maandamano hayo ikiwatahadharisha wananchi kutoshiriki kwa namna yeyote.

 

 

Kamanda Siro afunguka kuhusu 'kubomoa UKUTA'
Viongozi wa CUF wagoma kumpa mkono Profesa Lipumba