Siku moja baada ya rais wa awamu ya pili, Benjamini Mkapa kutoa kauli kali dhidi ya ngome ya Ukawa inayoundwa na vyama vikuu vya upinzani akiwaita ‘wapumbavu na Malofa’, Mgombea urais wa Ukawa, Edward Lowassa na mgombea mwenza Haji Duni wamezifikisha kwa wananchi.

Lowassa na Duni, jana walifanya ziara ya kushitukiza katika maeneo ya Gongo la Mboto na Chanika na kujumuika na wananchi wanaoishi katika maisha duni huku wakipanda daladala na kusikiliza matatizo ya wananchi.

Wakiwasalimu wananchi katika eneo la Gongo la Mboto, Haji Duni aliwaeleza wananchi kuwa hawakufika katika eneo hilo kufanya mkutano bali wanapita tu wakiwatembelea wananchi hao masikini wanaoitwa ‘wapumbavu na Malofa’, akirejea matamshi ya Mzee Mkapa.

“Haturuhusiwi kuzungumza zaidi, tukaambiwa tumefanya mkutano usiokuwa na ruhusa. Tumepita kuwasalimia wale masikini wanaoambiwa ni vibaka, malofa, wapumbavu,” alisema Haji Duni.

Ukawa wanatarajiwa kufanya mkutano wa uzinduzi wa kampeni Jumamosi, Agosti 29 mwaka huu katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.

Waziri Wa Mambo Ya Ndani Wa Zamani Akamatwa Na Kulala Selo
Mashabiki Wamkalia Kooni Rafael Benitez