Siku moja baada ya kujiunga rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa anatarajia kuchukua fomu ya kugombea urasi kupitia chama chake hicho, kesho.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Bw. Salumu Mwalimu ameviambia vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam kuwa mwanachama wao huyo mpya atachukua fomu ya kugombea nafasi ya urais kupitia chama hicho na kuongeza kuwa ni rukhsa kwake kuamua namna ya shamrashamra atakazokuwa nazo wakati wa tukio hilo.

Lowassa anategemewa kuwa mgombea rasmi wa kambi ya vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa iliyo na lengo la kukiondoa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ukawa watamtangaza mgombea wao Agosti 4.

 

Lukaku Aiweka Shakani Everton
Maelezo Ya Kina Kuhusu Job Ndugai Kumshambulia Kada Wa CCM Kwa Fimbo