Kwa mara ya kwanza watanzania wanatarajia kushuhudia mdahalo utakaowakutanisha uso kwa uso wagombea urais wa vyama viwili vyenye nguvu zaidi vya CCM na Chadema, Dk. John Magufuli na Edward Lowassa.

Mdahalo huo uliopewa jina la ‘Mkikimkiki 2015’ umeandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya TWAWEZA umepangwa kufanyika Oktoba 18 mwaka huu ili kuwapa nafasi wananchi kusikiliza sera za wagombea hao wakishindana kwa hoja uso kwa uso.

“Kupitia midahalo hii ya Mkikimkiki 2015 itatoa nafasi kwa vyama vya siasa kunadi ilani za vyama vyao na itawapa fursa wananchi kuwapima na kuwahoji wagombewa,” alisema Mshauri Mwandamizi wa Mawasiliano TWAWEZA,Risha Chande.

TWAWEZA wameeleza kuwa huo ni moja kati ya midahalo minne mikubwa ambayo itawakutanisha wagombea wa vyama mbalimbali vya kisiasa.

Hata hivyo, zoezi la kuwakutanisha wagombea urais wa Tanzania katika mdahalo liliwahi kushindikana mara kadhaa miaka iliyopita baada ya wagombea kutohudhuria kama ilivyotarajiwa

Magufuli Aiteka Mikoa Ya Kusini, Ni Mwendo Wa Tingatinga
Magufuli: Peoples Power, Nipeni Power Nilete Mabadiliko