Edward Lowassa ameshindwa kuvumilia kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuamua kuzitolea majibu.

Akizungumza jana katika ufungaji wa kampeni za ubunge wa jimbo la Arusha Mjini wakati anamnadi mgombea wa Chadema jijini humo, Godbless Lema, Lowassa alieleza kuwa amekuwa akikaa kimya pale anaposemwa vibaya lakini amelazimika kumjibu Kinana ambaye alidai kuwa kwenye kampeni zake alikuwa akizungumza dakika tatu tu kwenye kampeni.

Lowassa alisema alichokisema Kinana ni cha hovyo na kwamba alichotaka yeye kueleza ni kuwa Magufuli anatekeleza ilani ya Ukawa kwa kuwa umoja huo ndio uliokuwa ukieleza kuhusu matatizo ya reli na wizi wa viwanda.

Lowassa ambaye alikuwa mgombea urais kwa tikteti ya Chadema aliwataka wananchi wa jimbo hilo kumuaibisha Kinana kwa kumfanya ashindwe katika jimbo hilo ambapo ni nyumbani kwake.

“Mimi ninashangaa sana. Lakini kinana ni nani mpaka aseme hayo maneno? Nitamshangaa Magufuli kama ataendelea kumuweka Kinana madarakani wakati Arusha Nyumbani kwake ameshindwa vibaya,” alisema Lowassa.

“Nataka kura za kumuaibisha Kinana nyumbani kwake na tuhakikishe tunamfuta,” aliongeza.

 

 

Sumaye Akosoa Uamuzi Wa Rais Magufuli Kuhusu Wakwepa Kodi
Mwadui FC Yadhihirisha Stand Utd Si Lolote Kwao