Kada wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward ametamba kuwa bado anakitesa chama chake hicho cha zamani.

Akizungumza katika kikao cha ndani cha chama hicho mjini Iringa, Lowassa amesema kuwa kikao cha Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika mwaka huu mjini Dodoma alitajwa zaidi ya mara 360 kwa sababu ulikuwa mkutano wake.

“Pili uchaguzi Mkuu ujayo 2020 tutashinda tukiwa wamoja , tuwe wamoja na wanajua sisi ni wamoja . Mkutano mkuu CCM kule Dodoma walinitaja Mara 360 na zaidi , mkutano ule ulikuwa wa Lowassa kwa kuwa wanateshwa na jinamizi langu , linawatesa kweli kweli , kule nimetoka na CCM haipo tena nimeacha Lowassa na ndio sababu wanapata tabu kwa kuwa wanajua tumewashinda nchi hadi ndani ya chama chao,” alisema Lowassa.

Katika hatua nyingine, Lowassa alisisitiza kuwa chama chake kiko imara na kwamba lazima watafanya Oparesheni UKUTA kama walivyopanga ingawa alikiri kuwa na hofu pia.

“Hata Mimi nina hofu, lakini kama tusipotekeleza hili nchi itakuwa wapi hapo baadae. Haiwezekani mtu mmoja ajiamulie tuu kila jambo na kuvunja katiba,” alisema.

Alisema kuwa ingawa wako tayari kukaa katia meza ya mazungumzo, ni vyema wanaotaka kuwapatanisha pia waieleze Serikali kuhusu kinachofanyika kuzuia mikutano ya kisiasa kuwa ni kuvunja katiba ya nchi.

Mugabe aagiza wachezaji wa timu ya Olympic wakamatwe kwa kuboronga
Waziri wa Fedha Aigomea Polisi Nchini Afrika Kusini