Mgomnbea urais kwa tiketi ya Chadema anaeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa jana ametoa kauli mpya katika mkutano wake wa kampeni alioufanya katika jimbo la Monduli alilolitumikia kama Mbunge kwa kipindi cha miaka 20.

Lowassa aliwaeleza wananchi wa Monduli kuwa alichofanyiwa na Kamati Kuu ya CCM, Mjini Dododoma katika zoezi la kumtafuta  mgombea urais ulikuwa udhalilishaji na kwamba uamuzi wake wa kukihama chama hicho ulikuwa sahihi, huku akihoji waliotaka aendelee kubaki, “mlitaka Nife?”

Aidha, Lowassa alimzungumzia mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Namelock Sokoine,  na kueleza kuwa ingawa yeye ndiye aliyemshauri kugombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, hataweza kumuunga mkono akiwa CCM kwa kuwa alimshauri tena ahamie Chadema lakini alikataa. Alitumia muda huo kumpigia debe mgombea ubunge wa Chadema, Julius Karangaraiza.

“Ni kweli Namelock nilimshauri agombee ubunge kupitia CCM katika jimbo la Monduli. Lakini mabo yavyobadilika nilipohamia Ukawa nikamshauri tena ajitoe CCM lakini alikataa. Kama CCM hawatutaki watu wa Monduli kwa nini yeye aendelee kubaki? Mimi nimepanda basi la Chadema, na rafiki yangu yoyote anapaswa kupanda basi la Chadema,” alisema.

Katika hatua nyingine, Lowassa aliwahakikishia wananchi wa jimbo la Monduli kuwa hatakaacha kuendelea kutafuta tiba ya matatizo ya ardhi na matatizo mengi katika jimbo hilo. Alisisitiza kuwa wataendelea kupambana na kuwatetea watu wa Monduli kuhakikisha wanapata haki zao hata kama sio mbunge wa jimbo hilo, “tupo na tupo hai.”

 

Mwenyekiti Chama Cha Walimu Chato Aliyepanda Jukwaani La Lowassa Ashtakiwa
Jose Mourinho Aharibu Tena FA