Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa jana alikuwa Zanzibar ambapo alikamilisha ziara yake ya kutafuta wadhamini nchini.

Lowassa ambaye aliambatana na viongozi wa Ukawa, alitoa ahadi zake mbele ya umati mkubwa uliojitokeza katika viwanja vya Kibanda Maiti. Alisema endapo atapewa ridhaa na watanzania, kwa kushirikiana na Maalim Seif (Mgombea urais Zanzibar), atahakikisha anatatua matatizo ya muungano, ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na wizi wa kura wakati wa uchaguzi.

“Lakini nataka kuwaomba wazanzibar, na watanzania kwa ujumla kuwa uhakika wa kuitoa CCM madarakani tunao. Hatutawaondoa hivihivi, wanapenda madaraka na watang’ang’ania madaraka sana. Lazima tujiandae vizuri. Kazi iliyopo ni kwenda kupiga kura, ikulu hauendi kwa miguu…unakwenda kwa kura,” alisema Lowassa.

“Mkinipa nchi mimi na Maalim Seif, nchi itakwenda kwa speed ambayo haijawahi kutokea kimaendeleo. Hatuwezi kushindwa na Malawi, hatuwezi kushindwa na Rwanda na Burundi.”

Kwa upande wa mgombea mwenza wa Lowassa, Juma Haji Duni na Mgombea urais wa CUF, Maalim Seif Sharif waliwataka viongozi wa dola kuacha kuwatisha wafanyakazi wa taasisi hizo kuwa watapoteza kazi endapo Ukawa itaingia madarakani.

Ramos Akinzana Na Vyombo Vya Habari
CCM Yawatupa Nje Mawaziri Watatu, Majimbo Tisa Yapata Majibu