Mjumbe wa kamati Kuu Chadema Mh. Edward Lowassa amesema kuwa kazi ya siasa ni kuzungumza hivyo hakuna haja ya serikali kupata gadhabu juu ya matamko ya vyama vya upinzani kuhusu kufanya maandamano.

Wakati akifanya mahojiano na Azam Two  Mh. Lowassa amesema kuwa Serikali inapaswa kutambua kazi ya siasa ni kuzungumza hivyo siyo vyema kusema kuwa milango ya siasa kuwa inafungwa mpaka 2020, hivyo kutaka serikali itumie busara katika kuzungumza na upinzani juu ya kutafuta ufumbuzi wa jambo hilo.

”siasa ni kuzungumza hivyo tuzungumze, huwezi kuendesha chama cha siasa kwa kukifungia nadhani tukizungumza kabla ya tarehe 1 septemba muafaka unaweza kupatikana hakuna ambacho tutashindwana,nimesoma gazeti kuwa rais ataenda kahama kuwashukuru wananchi kwanini mimi nisiende Iringa na Mbeya kufanya kazi hiyo hiyo? Hakuna mtu mwenye hatimiliki ya nchi.” alisema lowassa.

Hata hivyo ameusifu utendaji kazi wa Rais Magufuli, Mh Lowassa amesema ni kazi nzuri Rais Magufuli anayofanya lakini ni vyema serikali iangalie na kulipa kipaumbele zaidi suala la kuzalisha ajira kwa vijana wote nchini ikiwa ni pamoja  na wahitimu wa vyuo tofauti na hayo mengine yanayoendelea kufanywa.

Aidha ameongeza kuwa Rais anatakiwa  asaidiwe kufuata utaratibu wa kuheshimu mihimili kwani nchi inaongozwa kwa kufuata mihimili mikuu mitatu yaani, Mahakama , Bunge na ,Serikali.

Lukuvi Atatua Mgogoro Wa Ardhi Magomeni Kota
Video: Mkia wangu uko pale pale - James Lembeli