Kiungo wa klabu ya Real Madrid, Luca Modric anakaribia kuweka rekodi ya kudumu kwenye timu ya Taifa ya Croatia baada ya kuiongoza kutinga Fainali kwenye UEFA Nations League, usiku wa kuamkia jana Alhamis.

Croatia walishinda 4-2 kwenye muda wa ziada kufuatia sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 90 dhidi ya wenyeji wao, timu ya Taifa ya Uholanzi.

Kwa sasa kikosi cha Zlatko Dalic kinasubiri mshindi kati ya Italia na Hispania ili kucheza nao fainali itayopigwa keshokutwa Jumapili (Juni 18), huku Waholanzi wakitarajiwa kucheza kuwania mshindi wa tatu.

Kama watachukua Kombe la UEFA Nations League hilo litakuwa kombe la kwanza la kimataifa kwa Modric ambaye alifunga bao dk 116 na timu yake ya Taifa ya Croatia.

Hii inakuwa fainali ya pili kwa Crotia kwenye mashindano makubwa baada ya 2018 kucheza fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa.

Kocha wa Croatia, Dalic alisema: “Tuna shaba na fedha, twende tukatafute dhahabu ili tumalize hadithi hii.”

Maboresho sekta ya Utalii yapo njiani - Mwigulu
Bruno Gomez mambo magumu Simba SC