Mshambuliaji wa Olympique de Marseille Dimitri Payet amefungiwa michezo minne, kufuatia tukio la kumtusi mwamuzi wakati wa mchezo wa ligi ya Ufaransa dhidi ya Montpellier mwishoni mwa juma lililopita.

Payet alionyeshwa kadi nyekundu dakika za mwisho, baada ya kuzozana na mwamuzi baada ya kuchukua maamuzi dhidi ya timu yake, ambayo ililazimishwa sare ya bao moja kwa moja.

Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka nchini Ufaransa (FFF), imepitia ripoti ya mwamuzi Amaury Delerue, na baadae kujiridhisha kupitia picha za televisheni kuhusu tukio hilo.

Kufuatia ahdabu hiyo, Payet atakosa mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Rennes, na ataendelea kuwa nje ya uwanja dhidi ya Amiens SC na PSG.

Biashara United yaachana na Amri Said
Wanao panga njama za kuipindua Serikali wakamatwa na milipuko